
Ndege mjanja hunaswa kwenye tundu bovu, unaweza kutumia akili nyingi kufanikisha tukio lako haramu na bado ikageuka kuwa kituko cha ajabu pindi utakapokamatwa!
Mwanamke
mmoja mwenye umri wa miaka 48, raia wa Thailand alikamatwa na maafisa
wa idara ya uhamiaji na mipaka wa Marekani katika mpaka wa Marekani na
Mexiko akiwa amejificha/amefungiwa ndani ya begi la nguo ili aweze
kuingia Marekani kinyamela.
Maafisa
uhamiaji wa Marekani waliweka wazi picha zinazomuonesha mama huyo
aliyefahamika kwa jina la Pornkamol Mongkolsermsak akiwa kwenye begi
lililokuwa nyuma ya gari lililokuwa linajaribu kuvuka mpaka.
Msemaji
wa CBP (Customs and Border Protection), Victor Brabble aliiambia CNN
kuwa tukio hilo lilitokea December 30 wakati maafisa walipolishtukia
gari aina ya SUV na kulifanyia ukaguzi kwa mara ya pili, ndipo
walipomkuta mama huyo akiwa amejificha chini ya nguo ndani ya begi.
Hata
hivyo maafisa hao hawakulitaja jina la dereva wa gari hilo aliyetajwa
kuwa na umri wa miaka 56, na wawili hao walifunguliwa mashitaka.
@
0 comments:
Post a Comment