Beyonce amejitetea kwa kutumia audio kutoka kwenye chombo cha angani cha Challenger kwenye wimbo wake XO.
Chombo hicho kililipuka January 28, 1986 sekunde 73 baada ya kuruka
Wajane
wa makamanda wa Challenger wamedai kusikitishwa na kitendo hicho cha
Beyonce ambaye hata hivyo amesema ametumia sauti hiyo kama heshima kwa
makamanda hao.
Wimbo
huo uliopo kwenye album yake mpya,'Beyonce' unaanza kwa kusikika sauti
ya ofisa wa NASA Steve Nesbitt akisema: "Flight controllers here looking
very carefully at the situation. Obviously, a major malfunction."
"Waandishi
wa wimbo waliweka sauti hiyo kama heshima kwa kazi ya crew ya
Challenger kwa matumaini kuwa hawatasahaulika,” alisema Beyonce kwenye
maelezo yake.
"Moyo
wangu uko pamoja na familia ya wale waliopoteza maisha kwa janga la
Challenger. Wimbo 'XO' ulirekodiwa kwa lengo la wazi kuwasaidia
kuwaponya waliopoteza wapendwa wao na kutukumbusha kuwa vitu
visivyotarajia hutokea, hivyo penda na kushukuru kila dakika uliyonayo
na wale wenye maana kubwa kwako,” alisema Bey.
Baadhi
ya mashairi kwenye wimbo huo yanasema: We don't have forever, Baby
daylight's wasting. You better kiss me before our time is run out."
0 comments:
Post a Comment