
Jeuri ya pesa inaonekana kwa couple ya Jay Z na Beyonce ambayo imetajwa kuwa imeingiza mkwanja mrefu zaidi kuliko couple yoyote ya wanamuziki.
Ijumaa
(December 27), wawili hao walitumia kiasi cha $100,000 (zaidi ya
shilingi milioni 158 za Tanzania) kwa ajili ya kununua vinywaji katika
club ya usiku ya ‘Rein’ huko Atlanta.
Kwa
mujibu wa TMZ, wawili hao walitumia kiasi hicho cha pesa kuwanunulia
vinywaji watu wote waliokuwa VIP, ambapo wasanii wenzao kama Bow Wow,
Jermaine Dupri, Dream na Trey Songz walikuwa miongoni mwa watu waliokuwa
VIP kuwapa kampani.
Jay-Z
na Beyonce walikuwa wakipongezana kufuatia kufanikiwa sana kwa album ya
Beyonce aliyoipa jina lake, lakini pia kutajwa kwa Jay-Z kuwania tuzo
ya Grammy katika vingele 9.
Katika
habari nyingine, Queen Bey amefunguka katika videoya Part 3 Run ‘N
Gun’, na kusema kuwa yeye na producer wa Drunk In Love walikunywa pombe
‘Dusse’ wakati wanarekodi ngoma hiyo, na kwamba ni kama alifanya
freestyle kwenye verse.
“Ni
kama nilifreestyle ile verse, na Jay akaingia na akaanza kuflow verse
yake.” Amesema Beyonce. “Ni kama tulikuwa na party. Ilikuwa poa sana,
kwa sababu hakukua na ubinafsi, hatukuwa tunajaribu kufanya hit ,
tulikuwa tunajaribu kufurahi na nadhani unaweza kusikia kwenye wimbo.”
Ameongeza.
Drunk
in Love ni wimbo unaopatikana kwenye album yake ‘Beyonce’ ambao
amefanya na mumewe Jay Z, video ya wimbo huo ina shots kadhaa zenye
mvuto wa mahaba zilizochukuliwa ufukweni.
0 comments:
Post a Comment