Muimbaji
wa Kigoma Allstars na hitmaker wa Kimugina, Linex Sunday amemlilia
model wa video za muziki nchini, Jackie Cliff kwa kusema kuwa kwake
ndiye model bora zaidi kuwahi kumpata.
Jackie
ambaye anaonekana kwenye video ya Kimugina, alikamatwa huko Macau,
China na madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya zaidi ya
shilingi milioni 220 na hadi sasa bado anashikiliwa huko.
“She' s ma best model I ever had#in God we trust#wethevoa,” ameandika Linex kwenye picha ya Jackie aliyoiweka kwenye Instagram.
Hivi karibuni, Linex alidai kuchoshwa na maswali anayoulizwa kuhusu mrembo huyo.
“Nimechoka
maswali kuhusu jack cliff model nilieshoot nae kimugina napenda
kuwambia wote wanaoniuliza maswali ya ajabu kwamba sijawah kuwa na
ushikaji na jack zaid ya kumtafuta nilipokua na kazi nae so sijui kitu
chochote kuhusu jack anafanya nn ana nn ana kaz gan zaid ya umodel sijui
so mnaonitupia maswali na picha wats up plzzz cos sijawahi kua karibu
na Jack na sijui chochote kuhusu jack zaidi ya kufanya nae video,”
aliandika kwenye Facebook.
0 comments:
Post a Comment