Ile
record label maarufu ya muziki afrika mashariki - candy n candy
imechapa fimbo nyingine baada ya kufanya deal ya mtonyo mrefuu na
kampuni maarufu ya kusambaza filamu afrika mashariki
na kati, (Jina kampuni ) kwa ajili ya kusambaza filamu ya “The gal
bladder” ambayo imechezwa na mwigizaji baby madaha akishirikiana na
waigizaji wengine toka kenya.
Kama
alivyonukuliwa toka mtandao mmoja maarufu wa habari Afrika Mashariki,
msemaji wa kampuni hiyo amesema imekua neema kwao kufanya kazi na
kampuni kubwa kama candy n candy films ya nchini kenya, na hiyo itapanua
wigo wa ukuaji wa tasnia ya filamu afrika mashariki hususani kenya na
tanzania..deal hiyo yenye thamani ya shilingi za kitanzania milioni mia
mbili ( mil.200 )inakua moja ya mikataba minono zaidi kufanywa east
africa kutoka kwa kampuni kwenda kwa kampuni kwenye upande wa filamu.
Hiyo
inachukukuliwa kuwa moja la pigo la kukata na shoka kwa kampuni
pinzani grandpa records nayo ya nchini kenya ambayo kwa muda mrefu
imekuwa ndani ya tasnia ya burudani kwa takribani zaidi ya miaka kumi
bila kuleta mabadiliko yoyote katika tasnia nzima ya burudani,jambo
ambalo candy n candy imeweza kufanya ndani ya miezi mitano tu,katika
kutengeneza muziki wa kimataifa bila kusahau project yao ya sasa “highly
budget movie the gal bladder”….ni mfano wa kuigwa kutoka kwa candy n
candy records label kuzalisha kampuni tanzu ndani yake ya candy n candy
films ambayo itakuwa ikidili na filamu.
Mbali
na hayo kampuni hii ina plans za kuanzisha kipindi matata cha runinga
ambacho kitakua kikirushwa Afrika Mashariki yote ,ambapo kama kawaida
huwa hawachezi mbali host wake atakua first lady wa candy n candy
mwanamuziki,mwigizaji,mwanamitindo na mtangazaji baby madaha”the queen
of swaggz”,ikumbukwe hivi karibuni alilamba mamilioni ya shilingi
kupitia mkataba wake na kampuni hiyo.

0 comments:
Post a Comment