Muigizaji wa kike nchini, Rose Ndauka amesema hakuna raha kubwa duniani kama ile anayojisikia mwanamke pindi awapo mama.
Ndauka
aliyejifungua mtoto wa kike Desemba 29 katika hospitali ya taifa
Muhimbili amesema kwa muda mfupi tangu ajifungue anajiona amebadilika
kihisia.
"Hakuna
raha kama kuwa mama. Napatwa na hisia za ajabu, huwezi amini mimi
nilikuwa mlalafi mno, lakini sasa hivi pindi mtoto wangu anapoamka hata
kabla hajalia naamka ghafla na kumsaidia au kumnyonyesha nashangaa
inakuwaje nina hisia za ajabu kuhusu mtoto wangu akili tu siwezi fanya
kitu kingine jicho langu lote linatua kwake," Ndauka ambaye amezaa na
muimbaji wa kundi la TNG Squad, Malick Bandawe aka Chiwa Man ameliambia
gazeti la Mwananchi.
0 comments:
Post a Comment