13:37
1. Wivu Wa Kupindukia
Ni Jambo Jema Kwa Mwanamume Kumtakia Heri Mpenzi Wake Na Kufanya Kila Awezalo Kuhakikisha Kuwa
Hapati Madhara, Lakini Iwapo Utakuwa Mtu Wa Wasiwasi Na Mashaka Pale
Unapomwona Mpenzi Wako Akizungumza Na Mwanamume Mwingine, Au Anapotoka
Na Marafiki Zake Wa Kike, Au Anapovaa Nguo Inayomfanya Atamanishe, Basi
Fahamu Kuwa Tayari Umekunywa Sumu Ya Mapenzi.
Katika
Uhusiano Wa Kimapenzi, Kuaminiana Ni Jambo Muhimu Sana. Kama Kweli
Unataka Mpenzi Wako Akupende Kwa Dhati, Mwoneshe Kuwa Unamwamini Na
Unaheshimu Maamuzi Yake, Ikiwa Ni Pamoja Na Maamuzi Ya Kutoka Na
Marafiki Zake Wa Kike Na Kuwa Na Marafiki Wa Kawaida Wa Kiume. Ondoa
Hofu Na Acha Kabisa Kumpeleleza, Maana Wapo Wanaume Ambao Hutumia Muda
Wao Mwingi Kuwapeleleza Wapenzi Wao Ikiwa Ni Pamoja Na Kuwategeshea
Kamera Na Rekoda Za Simu.
2. Kutomwachia Nafasi Mpenzi
Kama
Huishi Na Mpenzi Wako Ni Jambo La Kawaida Kuwa Na Hamu Ya Kumwona Mara
Kwa Mara, Lakini Kumbuka Kuwa Mpenzi Wako Naye Ana Maisha Yake Na
Anahitaji Nafasi Ya Kuwa Peke Yake Kwa Ajili Ya Mambo Yake Binafsi.
Hisia
Za Kutaka Kuwa Na Mpenzi Wako Muda Wote Zinaweza Kudhaniwa Kuwa Ni Za
Mapenzi Ya Dhati, Lakini Kwa Hakika Hiyo Si Ishara Njema Ya Mapenzi Ya
Kudumu. Hebu Jiulize Kama Unaweza Kuendeleza Hali Hiyo Maisha Yako Yote.
Ni Wazi Kuwa Utachoka. Kwa Hiyo, Mpe Mpenzi Wako Fursa Ya Kupumua.
Namna Hii Mpenzi Wako Atajenga Hamu Ya Kutaka Kukutana Nawe Lakini Ukiwa
Naye Muda Wote Hamu Hiyo Itaisha.
3. Kumwamulia Mpenzi Mambo Yake
Unaweza
Kujikuta Ukisukumwa Kumwambia Mpenzi Wako Awe Anavaa Nini Wakati Gani,
Akutane Na Nani Na Kwa Wakati Gani Au Ale Nini. Ukiona Hivyo, Fahamu
Kuwa Hayo Si Mapenzi, Bali Umepitiliza Na Pengine Mwisho Wa Uhusiano
Wenu Unanukia.
Hata
Ukiachilia Mbali Suala Zima La Usawa Wa Jinsia, Hakuna Mwanamke Ambaye
Angependa Apangiwe Kila Kitu Kuhusiana Na Maisha Yake. Kama
Ilivyodokezwa Hapo Juu, Kila Mtu Ana Maisha Yake Na Kilichowaunganisha
Ni Mapenzi Tu. Kama Utataka Kumpangia Kila Kitu Ni Wazi Kuwa Utaishia
Kuishi Peke Yako.
4. Kumuuliza Mpenzi Maswali
Iwapo
Utajikuta Ukimuuliza Mpenzi Wako Maswali Mengi Yanayoonesha Wasiwasi
Wako Kuhusiana Na Mwenendo Wake, Fahamu Kuwa Kuna Tatizo Na Tatizo Hilo
Lisipopatiwa Ufumbuzi Utakuwa Mwanzo Wa Mwisho Wa Uhusiano Wenu.
Mwanamke
Angependa Umuulize Maswali Ya Kawaida Kuhusiana Na Jinsi Siku Yake
Ilivyokuwa Na Kama Marafiki Zake Hawajambo Au La, Lakini Kila Jambo Lina
Mpaka Wake. Mwanamke Hatarajii Kuwa Kila Mnapokutana Atakuwa Kama
Ameingia Kwenye Chumba Cha Mtihani Au Usaili Wa Kazi.
5. Kutoamini Anachokweleza Mpenzi
Wakati
Mwingine Watu Hushindwa Kuwaamini Wenzao, Lakini Kwa Sababu Ambazo Ni
Za Msingi, Lakini Kuna Wakati Ambapo Mtu Hushindwa Kumwamini Mwenzake
Bila Sababu Yoyote Ya Msingi, Au Kwa Sababu Zisizo Sahihi, Kisingizio
Kikiwa Ni Mapenzi.
Kuna
Tatizo La Kisaikolojia La Kujishuku Au Kuwashuku Wenzako. Hili Ni Jambo
Ambalo Linaweza Kukuharibia Mustakabali Wako Katika Mapenzi, Maana
Husababisha Kujengeka Kwa Mazingira Ya Kutokuaminiana. Ili Uweze Kwenda
Sanjari Na Mpenzi Wako, Amini Kila Anachokweleza Hadi Pale Utakapokuwa
Na Sababu Za Msingi Za Kutokumwamini. Na Hata Unapokuwa Umelithibitisha
Jambo, Endelea Kuwa Katika Uhalisia Wako.
6. Kuacha Hobi, Marafiki
Mahusiano
Ya Kimapenzi Mara Nyingi Huhusisha Kila Mmoja Kuacha Baadhi Ya Mambo
Yake Kwa Ajili Ya Mwenzake. Hata Hivyo, Lengo Ni Kuweka Tu Uwiano Wa
Mahitaji, Si Kuacha Kila Kitu Ulichokuwa Nacho Kwa Ajili Ya Mwenzako,
Ama Kwa Shinikizo, Au Kwa Kulewa Penzi.
Iwapo
Utabaini Kuwa Marafiki Zako Sasa Wamekuwa Ni Marafiki Zako Wa Zamani Na
Hobi Zako Zimebaki Tu Katika Kumbukumbu Japo Kwa Hakika Bado Unahisi
Mapenzi Katika Hobi Hizo, Basi Tambua Kuwa Huyo Mrembo Wako Amekunywesha
Sumu Ya Penzi Na Sasa Huwezi Hata Kuitumia Vema Mantiki Yako.
Mbaya
Zaidi, Iwapo Utabaini Kuwa Marafiki Zako Wapya Ni Marafiki Wa Siku Zote
Wa Mpenzi Wako Na Hobi Zako Ni Zile Za Mpenzi Wako, Basi Tambua Kuwa
Huna Tena Nafsi Yako, Bali Umejisalimisha Mzima Mzima Kwa Mpenzi Wako.
Lakini Msemo Mmoja Wa Hekima Unatwambia Usiweke Mayai Yako Yote Kwenye
Kikapu Kimoja. Yamkini Unaelewa.
7. Kukubali Kupelekeshwa
Pengine
Unakumbuka Kuwa Kuna Nyakati Ambapo Ulikuwa Na Uwezo Wa Kujikita Katika
Jambo Moja Na Kulifanya Kwa Umakini, Huku Ukiwa Pia Mwerevu, Mjanja Na
Unayejisimamia, Lakini Leo Unayeyuka Kirahisi Tu Kama Barafu Iliyowekwa
Juani! Hii Ni Hatari Kwa Mustakabali Wa Maisha Yako.
Mbaya
Zaidi Ni Pale Utakapoiacha Kazi Yako Inayokulipa Vizuri Na Kufanya Kazi
Nyingine Kwa Ajili Ya Kumfurahisha Mpenzi Wako. Ukifika Hali Hii Ujue
Wewe Mwenyewe Kuwa Hapo Hakuna Mwanamume.
8. Utayari Wa Kufa Kwa Ajili Yake
Umewahi
Kujisikia Kuwa Na Utayari Wa Kufa Kwa Ajili Ya Mpenzi Wako? Kama Jibu
Ni “Ndiyo”, Basi Fahamu Kwa Hakika Kuwa Hayo Uliyo Nayo Si Mapenzi Bali
Ni Upumbavu. Pengine Huku Ndiko Kunywesha Sumu Ya Mapenzi. Kwa Hakika,
Hakuna Mwanamke Ambaye Anastahili Kumfanya Mwanamume Yeyote Kufa Kwa
Ajili Yake.
Yamkini
Wanaume Wanaolengwa Katika Makala Haya Si Wavulana Wanaosoma Sekondari,
Waliobalehe Majuzi, Ambao Wakipenda Au Kupendwa Hujiona Kama Wako
Katika Sayari Yao. Mwanamume Aliyepevuka Hujiamini Na Hayaweki Maisha
Yake Yote Mikononi Mwa Mwanamke, Hata Kama Mwanamke Huyo Angekuwa Ndiye
Mrembo Wa Dunia.
Iwapo,
Ama Kwa Ujinga Au Kwa Kufahamu Umewahi Kumwambia Mpenzi Wako:
“Ukiniacha Nitajiua,” Na Ukawa Unaamini Hivyo Kabisa, Basi Yamkini
Unahitaji Kutafuta Msaada Wa Ushauri Nasaha, Maana Kwa Hakika Umepotoka.
9. Muda Wote Unawasiliana Naye
Vijana
Wa Siku Hizi Ni Watumiaji Wazuri Sana Wa Simu, Lakini Iwapo Utabaini
Kuwa Asilimia Kubwa Ya Muda Wako Unautumia Ama Kwa Kuongea Au
Kuwasiliana Kwa Ujumbe Mfupi Na Mpenzi Wako, Basi Fahamu Kuwa Kuna
Tatizo Ambalo Linahitaji Ufumbuzi Wa Haraka.
Kumbuka
Kuwa Mapenzi Hayachukui Nafasi Ya Kila Kitu. Yamkini Huyo Mpenzi Wako
Amekukuta Unaishi Na Kuna Mambo Ya Muhimu Ya Kufanya. Hebu Achana Na
Simu Kwanza Ufanye Mambo Ya Muhimu Kuhusiana Na Maisha Yako. Kama Mpenzi
Wako Hakwelewi Katika Hili Basi Hakufai.
10. Ndugu Zake Wanakufuatilia
Iwapo
Utabaini Kuwa Marafiki, Ndugu Na Jamaa Za Mpenzi Wako Wanamtonya Mpenzi
Wako Kuhusiana Na Kile Wanachokiita Mwenendo Wako Mbaya, Usipuuze Hali
Hii. Kuna Uwezekano Mkubwa Kuwa Watu Hawa Wanayo Sababu Ya Kuwa Na
Wasiwasi Na Mwenendo Wako, Kwa Hiyo Jichunguze Na Kuangalia Jinsi
Unavyoenenda.
Hata
Hivyo, Jambo Hili Si Ishara Njema Ya Mustakabali Mwema Wa Uhusiano
Wenu. Iwapo Mpenzi Wako Ataweka Watu Wake Wakufuatilie, Maana Yake
Halisi Ni Kwamba Hakuamini. Katika Hali Kama Hii, Haitarajiwi Kuwa
Mustakabali Wa Uhusiano Wenu Utakuwa Mzuri, Kwani Kutakuwa Na Uingilizi
Mwingi Wa Ndugu, Jamaa Na Marafiki Zake. Unaweza Kukubali Kuendelea
Kuishi Katika Hali Hii Kwa Kisingizio Cha Mapenzi, Lakini Ukweli Ni
Kwamba Hayatakuwa Mapenzi Bali Karaha.
KUWA MAKINI
Kama
Unavyoona, Hizi Ni Baadhi Tu Ya Dalili Kuwa Mapenzi Yako Kwa Mwanamke
Sasa Yanaelekea Katika Ulevi, Mithili Ya Ule Wa Dawa Za Kulevya. Jambo
Moja La Kukumbuka Ni Kwamba Kweli Mapenzi Ni Kitu Kizuri, Lakini Pia
Mapenzi Yanahitaji Kuwa Jambo Linaloashiria Mustakabali Mwema Kwa
Wahusika Wawili. Yakiwapo Mambo Haya Kumi Hauwezi Kuwapo Mustakabali
Mwema Katika Mapenzi.
0 comments:
Post a Comment