
Mwaka
2014 umeshaaanza ikiwa ni siku ya tatu, matukio muhimu katika kalenda
inabidi yapigiwe mstari ama kuwekewa alama yasisahaulike.
Mwimbaji
wa nyimbo nzuri za mapenzi Mariah Carey ametangaza kuwapa wapendanao
zawadi kwa kuachia wimbo wake mpya siku ya wapendanao aka Valentine’s
Day (February 14).
Mkali huyo wa Touch My Body alitangaza kwenye show aliyokuwa anafanya katika usiku wa mkesha wa mwaka mpya.
Alitumia
nafasi hiyo pia kuwaambia watu kuhusu ujio wa album yake inayosubiriwa
kwa hamu ‘The Art of Letting Go’ ambapo alisema itatoka katika mapema
iwezekanavyo aka punde ‘soon’.
“The album is coming this spring.” Alisema Mariah Carey. “New Single, Valentine’s Day.”Aliongeza.
Album
hiyo ya Mariah Carey ilitakiwa kutoka mwezi July mwaka jana, lakini
alisogeza mbele tarehe na kudai kuwa alitakiwa kuongeza nyimbo nzuri na
asingependa kuacha nyimbo zenye maana.
0 comments:
Post a Comment