Watu wawili wanashikiliwa na polisi nchini Tanzania baada ya kukamatwa na shehena ya meno
ya tembo katika bandari ya Dar es Salaam, waliyokuwa wakisafirisha kiharamu maafisa wa nchi hiyo wamesema.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Wizara ya Maliasili na
Utalii wa Tanzania, Chikambi Rumisha amesema meno hayo yapatayo 81 yana
uzito wa kilo 303.
Kwa
mujibu wa maafisa wa Wizara meno hayo ya tembo ni mapya ikiwa na maana
yametokana na tembo 41 waliouawa ndani ya mwezi mmoja uliopita.
Naibu
Waziri wa Maliasiali na Utalii wa Tanzania Lazaro Nyalandu amesema
mauaji ya tembo yameongezeka nchini humo baada ya operesheni ya
kupambana na majangili iliyopewa jina la "Operesheni Tokomeza"
kusimamishwa kutokana na baadhi ya watendaji kukiuka haki za binadamu.

0 comments:
Post a Comment