KWA muda mrefu, zilisikika sauti za kupiga vita
makundi ya wanawake yaliyosifika kwa kucheza utupu kwa kulowanisha
khanga maji maarufu kama Khanga Moko Ndembendembe lakini sasa imeibuka
nyingine, inayoitwa Fulana au Tisheti Ndembendembe.
Uchunguzi
wetu wa miezi kadhaa tangu mwaka jana ulibaini kwamba tayari staili
hiyo ya uchezaji wa muziki wa mwambao kwa kulowanisha tisheti laini
nyeupe kwa maji na kusababisha chuchu kuonekana sawia, inazidi kushika
kasi kama moto wa kifuu Bongo.
Ilibainika kuwa staili hiyo ambayo
ilianzia Pwani ya Kenya, sasa inatumiwa kudhalilisha warembo Uswahilini
hasa kwenye ngoma maarufu za ‘kigodoro’ ambazo huchezwa bila kujali rika
mbalimbali zinazokuwa zimechanganyikana. Habari zilisema kuwa katika
uchezaji huo, sharti ‘nido’ ya mrembo iwe saa sita ili kuwavutia na
kuwaridhisha wanaume kimahaba ambao kazi yao huwa ni kuwatuza fedha
baada ya kufurahishwa kwa kutazama uchezaji huo na wengine kuondoka nao
kwenda kuvunja amri ya sita.
Ilifahamika kuwa staili hiyo imewavutia wengi na vikundi vya uchezaji huo vimeanza kuundwa japo havijapata umaarufu mkubwa.
Mamlaka
na wizara husika zinatakiwa kukemea kwa nguvu zote kwani huo ni mwanzo
mwingine wa mmomonyoko wa maadili ya Kitanzania na ongezeko la
maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU).
Credits:habarizaudaku
0 comments:
Post a Comment