Mwaka 2013 umekuwa wa mafanikio makubwa kwa Rehema Chalamila aka Ray C. Kubwa anamloshukuru Mungu ni kuokolewa kutoka kwenye
maangamizi yaliyosababishwa na kuathirika na matumizi ya madawa ya
kulevya, thanks kwa Rais Jakaya Kikwete aliyeamua kugharamikia matibabu
yake.
Baada
ya matibabu hayo, muimbaji huyo wa ‘Niwe Nawe Milele’ amerejea kwenye
afya yake ya kawaida na sasa yupo busy kurekodi nyimbo mpya na huenda
mapema mwaka 2014 akarejea kwa kishindo. Pamoja na kupewa gari nzuri ya
kutembelea, Ray C ameionyesha nyumba yaka anayoijenga na iliyokamilika
kwa asilimia kubwa huku ikifanyiwa upambaji wa ndani tu.
Ray
C ameionesha nyumba yake kwenye Instagram kwa kuandika: Love the color
of ma new house!!!! Under construction #godisgood#workhardplayhard."
0 comments:
Post a Comment