Msanii
wa muda mrefu kwenye 'game' ya muziki nchini Kenya, Amani amweweka wazi
kuwa anajipanga kwaajili ya kuzindua ujio wake mpya na wa kishindo
katika tasnia ya muziki, sambamba na msanii Mr Lenny.
Tayari
Amani amekwishafanya kazi kadhaa kali chini ya lebo mahiri ya Grandpa
ya huko huko nchini Kenya, ambao watasaidia kwa nafasi yao kumrudisha
Amani katika level yake.
Amani
na Mr Lenny ni kati ya wasanii ambao wanashikilia rekodi ya kutikisa
sana tasnia ya muziki katika miaka iliyopita, kabla ya kutulia kwa muda
wakiwa wanafanya shughuli nyingine pembeni ya muziki.
0 comments:
Post a Comment