Tuesday, 31 December 2013

Ijue sababu ya kwanini Lady Gaga asingefanikiwa bila Akon.


Mwaka 2006, Lady Gaga  alikuwa msanii mchanga aliyekuwa akijulikana kwa jina lake Stefani Joanne Angelina Germanotta.

Kipindi hicho, Germanotta alikuwa na miaka 19 alikuwa akisafiri kwa basi kutoka  New York City kwenda  Parsippany, New Jersey siku saba za wiki kufanya kazi na producer aitwaye Rob Fusari.
Kila siku Stefani alipokuwa akiingia kwenye studio,  Rob alikuwa akicheza wimbo uitwao ‘Radio Gaga wa Queen, kama wimbo wake wa kuingilia. Siku moja alikuwa akikuna kichwa kutafuta jina la utani,  Fusari  akamtumia sms kupendekeza jina "Radio Ga Ga" lakini masahihisho ya simu (autocorrect) yakalibadilisha jina na kujiandika "Lady Ga Ga". Stefani akajibu pale pale: Hilo ndo lenyewe. Hili ndio jina langu jipya. Usiniite Stefani."
Katika kipindi hicho ameenza kujiita Gaga, alikuwa akifanya kazi kama mwandishi wa nyimbo kwenye  Streamline records, kampuni ya  Jimmy Iovine wa  Interscope records. Stefani  aliwaandikia nyimbo wasanii wakubwa kama Britney Spears na Fergie.
Siku moja  Akon alikuwa akihangaika kuandika nyimbo kwaajili ya albam yake ya pili "Konvicted". Stefani aliombwa kwenda studio na kuimba sauti atakazotumia Akon. Akon aliguswa na uimbaji wa Gaga kiasi ambacho aliacha kurekodi na kwenda moja kwa moja kwenye ofisi ya Jimmy Iovine na kumshawishi amuachie Stefani amsainishe kwenye label yake Kon Live.
Akon akaanza kuchangia pia sauti kwenye nyimbo kadhaa za kwenye albam ya kwanza ya Gaga, "The Fame" na pia alishiriki kuandika wimbo wake wa kwanza uliomtambulisha, "Just Dance".
Kwenye interview aliyofanya mwaka 2011, Akon alikiri kuingiza fedha kupitia Lady Gaga mara 10 zaidi ya kazi zake mwenyewe.

0 comments:

Post a Comment