
Sera
ya Tanzania ya Kilimo Kwanza inafanyiwa kazi kivitendo na familia ya
kifalme ya Uingereza ambapo Prince William ameamua kurudi chuo kusomea
masuala ya kilimo.
Uongozi
wa familia hiyo umetoa tamko rasmi jumatatu (December 30), kwamba
Prince William atajiunga na chuo kikuu cha Cambridge (Cambridge
University) na kusomea maswala ya kilimo kuanzia January hadi March.
“Kozi
hiyo imeandaliwa kusaidia kumpa uelewa kuhusu mambo yanayoendelea
kutokea yanayoathiri biashara ya kilimo na jamii za vijijini ndani ya
Uingereza.” Utawala huo umeeleza.
Hata
hivyo, Prince William ambaye ni baba wa mtoto mmoja ataendelea na
majukumu mengine kama kawaida yanayohusu familia hiyo ya kifalme.
Prince William alihitimu shahada ya kwanza ya masomo ya Jografia , St. Andrews University mwaka 2005.
Pia aliwahi kujiunga na mafunzo ya Jeshi na kujikita katika maswala ya uokoaji.
0 comments:
Post a Comment