Steve Mangere ‘Steve Nyerere’.
Stori: Nyemo ChilonganiWAIGIZAJI wawili kwenye tasnia ya ya filamu Bongo, Steve Mangere ‘Steve Nyerere’ na Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ wapo katika mvutano wa
hali ya juu kufuatia kila mmoja kutangaza nia ya kugombea uenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie.
Imeelezwa kuwa, katikati ya wiki iliyopita wasanii hao walikutana katika pati ya Baby Madaha iliyofanyika Posta jijini Dar, ambapo kila mmoja alijinadi kumfunika mwenzake katika nafasi hiyo, hivyo kuzua minong’ono na kuwagawa wasanii, wengine walimuita Steve Nyerere Mwenyekiti, wengine walimuita Dk Cheni.
“Mh! Hivi leo ni vikumbo vya waziwazi maana Steve anajinadi kivyake, mbona hapatoshi tuusubiri huo uchaguzi tuone nani ataibuka kidedea,” alisema msanii mmoja, aliyeomba hifadhi ya jina.
Credit-GPL


0 comments:
Post a Comment