Monday, 6 January 2014

Barnaba kutafuta wasanii wawili watakaokuwa chini ya label ya studio yake mpya aliyoianzisha.

Mwimbaji wa Bongo Flava, Barnaba Elias aka Barnaba Boy amepanga kuwatafuta wasanii wawili wapya katika muziki wa kizazi kipya ambao watakuwa chini ya label ya studio yake binafsi aliyopanga kuitambulisha rasmi kwa mashabiki wake.

Mwimbaji huyo wa ‘Sorry’ ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa anahitaji kuwa na wasanii hao wawili kwa kubalance jinsia, mmoja wa kike na mmoja wa kiume ambao atasimamia kazi zao za muziki kama meneja wao.
“Kila kitu kina mipango, kwa sasa nimeshafanya maandalizi ya studio yangu mpya ambayo soon tu mashabiki wataanza kusikia kazi mbalimbali. Pia natarajia kusaini wasanii wawili (wa kike na wa kiume) ambao kazi zao nitakuwa nikizisimamia.” Amesema Barnaba Classic.
“Research yangu nitaianza wakati wowote kuwatafuta wasanii hao wawili hapa Dar es salaam.” Ameongeza.
Hata hivyo, Barnaba amesema bado hajaamua jina litakalowakilisha studio yake na label yake.

0 comments:

Post a Comment