Sunday, 5 January 2014

Brigitte Alfred (Miss Tanzania 2012): Nawekeza hela yangu kwenye ardhi.


Wakati ambapo mastaa wengi wa kike wa Dar es Salaam wanakimbilia kununua magari ya
kifahari, Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred anafikiria tofauti. Mrembo huyo anawekeza hela yake kwenye ardhi.
Brigitte amepost picha kwenye Instagram inayomuonesha akiwa kwenye kiwanja anachokinunua/alichokinunua huku akiwa na watu wawili wanaomuonesha kitu kwenye karatasi.
“Putting my money on such investments-land..early morning surveying,” ameandika kwenye picha hiyo.

0 comments:

Post a Comment