
Siku kadhaa baada ya DMX kuanza kupiga shows zitakazomsaidia kupona vidonda vya kufulia, mkali huyo ameendelea kushikilia imani yake na kupiga maombi na timu yake yote kabla hajafanya show ili mambo yaende sawa.
Kiongozi
huyo wa zamani wa Ruff Ryders ameonekana katika kipande kifupi cha
video akiomba kwa jina la Yesu zisitokee fujo za aina yoyote katika
tamasha alilokuwa anafanya katika jiji la Detroit, jiji ambalo jarida la
Forbes limelitaja kama ‘jiji hatari zaidi Marekani’.
Katika
kipande hicho kilichooneshwa na TMZ, anaonekana DMX akiwaaambia watu
wake wasali na kushikana mikono kwa pamoja na kuinamisha vichwa vyao
chini kwa ajili ya maombi.
“Tafadhali Mungu usiruhusu mtu yeyote asumbuliwe ama apigwe risasi.” Ni moja kati ya maneno aliyoyaomba DMX katika sala yake.
“Tunaomba
kwamba kusitokee ugomvi, kujeruhi, ufyatulianaji risasi, wala mtu
kukamatwa, majibizano ya ugomvi wala vitendo vinavyofanana na hivyo.”
Aliomba DMX.
Maombi
ya DMX yalisikika na hatimaye show ilifanyika kwa amani na hakuna
kitendo chochote cha uhalifu kilichoripotiwa katika show hiyo.
0 comments:
Post a Comment