Mkali wa Pop, Britney Spears anaripotiwa kuwakwaza mashabiki wake waliokuwa na kiu ya kukutana na kupiga picha
Fans hao waliokuwa wamejipanga
kukutana na star huyo na kupiga naye story, walijikuta katika wakati
mgumu baada ya kupewa sekunde 3 kwa ajili ya kuweka pozi na kupiga naye
picha tu.
“Mashabiki waliambiwa kabla kuwa
katika kukutana naye hawaruhusiwi kumgusa wala kumkumbatia bila ruhusa
yake na hawakuruhusiwa kumpelekea zawadi yoyote. Na hatimaye
walipofanikiwa kukutana naye ilikuwa kama ‘tabasamu, piga picha,
kwaheri. Kila mmoja alipata kama sekunde 3 kuwa naye.” Chanzo kimoja
kiliuambia mtandao wa Radar Online.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa Britney
ni kama hakuongea nao, alikuwa na sentensi moja tu kuwaambia baada ya
kupiga picha huku akitabasamu, “Thank-you a lot.”
0 comments:
Post a Comment