
Mrembo wa Namibia na mshindi wa Big Brother Africa The Chase, Dillish amemnunulia
mwakilishi
wa Ghana kwenye shindano hilo la mwaka jana, Elikem, pikipiki ya
kifahari yenye thamani ya dola za Kimarekani 14,000 ambazo ni zaidi ya
shilingi milioni 22 za Tanzania.
Wawili
hao walikuwa wameahidiana kununuliana zawadi kama mmoja wapo angeshinda
ambapo Dillish alimuahidi Elikem kumpa pikipiki na Elikem alimuahidi
mrembo huyo kumnunulia gari kama angeshinda. Na wiki hii Dillish
ametimiza ahadi yake kwa kumnunulia pikipiki hiyo aina ya Suzuki GSXR
1000.
Dillish
alipost picha ya pikipiki hiyo kwenye Instagram na kuandika: "Finally
got my brother the bike he said he would buy if he won. We made a bet on
this and I am a woman of my word. Enjoy it buddie and be SAFE!!!"
Elikem alitweet akisema: @Dillish_lishy . thanx hun. U kept ur word. LOVE LOVE all over u".
0 comments:
Post a Comment