Kauli ya Chadema juu ya kesi baina yao na Zitto Kabwe.
baada ya jaji kuahirisha kesi hii ambayo imeonekana ina msuguano wa kisheria pande zote mbili,upande wa Chadema waliweka mawakili watatu Peter Kibatala,John Marya wakiongozwa na wakili wa Chadema Tundu Lissu
Upande
wa Zitto Kabwe alikuwa na wakili mmoja tu ni Albert Gasper Msando
ambaye pia ni diwani wa kata ya Mabogini kupitia Chadema huko 87.9
Moshi,millardayo.com imeongea na Tundu Lissu kama Wakili wa Chadema na
hiki ndicho alichokisema.
‘Nafikiri tumeenda vizuri pande zote
mbili zimepigana kwa ufundi mkubwa sana nafikiri Jaji ana kazi kubwa
sana kesi imehairishwa mpaka Jumatatu kwa sababu masuala yaliyojadiliwa
ni masuala mazito sana kisheria yanahitaji muda wa Jaji kufanya utafiti
na kuyatafakari’
‘Nawaambia wanachadema chama chetu
kipo imara hili wingu litapita lakini ni muhimu wanachama wafahamu
mahali ambapo tumefika leo chama lazima kisafishe uchafu wote ndani ya
chama utovu wote wa nidhamu uondolewe chama lazima kijisafishe
vinginevyo hatutoweza kama tutaendekeza usaliti na kelele za aina
hii,ujinga wa aina hii chama kitasamabaratika’
‘Mimi sidhani kama kuna makundi
mawili,kwenye kamati kuu nzima wajumbe zaidi ya 30 wote wameungana na
hicho ndio chombo cha juu kabisa cha kufanya maamuzi ya chama,kuhusu
baraza kuu kikao cha mwisho kabisa cha mwaka jana januari.
‘Mwenyekiti wa chama ilibidi azime
mjadala uliokua kwenye baraza kuu kumhusu mheshimiwa Zitto Kabwe,wajumbe
wa baraza kuu walikua wanasema huyu mtu aondoke toka mwaka jana kwa
hiyo haya maneno kuwa baraza kuu tunaenda kushinda ni maneno yale yale
kwamba kwenye kamati kuu tupo wengi tuna akili nyingi hawatotugundua
tumesoma hawa wengine hawajasoma akili ndogo’.
‘Suala la uanachama halipo baraza kuu
suala la uanachama lipo kwenye kamati kuu kwenye baraza kuu anapeleka
rufaa kwamba ameadhibiwa kimakosa amevuliwa nyadhifa zake kimakosa hivyo
uanachama wake unajadiliwa kwenye kamati kuu’@mndewa

0 comments:
Post a Comment