
Miaka
ya 90 kurudi nyuma ilikuwa nadra sana kukuta mwanamke ana
kitambi.Ukimkuta mwanamke anatumbo kubwa wakati huo, lazima atakuwa ana
mimba.
Hali
sasa inatisha. Wanawake wengi wana vitambi kiasi kwamba ni vigumu
kutofautisha wenye mimba na wasio kuwa na mimba. Wengi ninao kutana nao
barabarani, sehemu za umma, ninaokutana nao maofisini na sehemu mbali
mbali nimegundua kuwa kati ya wanawake 10, 7 hadi 8 wana vitambi au
matumbo makubwa. Wengine vitambi vyao ni vikubwa na vingine vinakuwa
vimevimbiana pembeni yaani upande wa kushoto na kulia ubavuni hivyo kuwa
na umbo kama la matumbo ya vyura. La ajabu ni kuwa wanaume wengi sasa
hivi hawana vitambi isipokuwa walafi wachache. Kwakuwa zamani tulizoea
kuwa vitambi ni kwa wanaume sasa hali imebadilika imekuwa ni wanawake.
Nini kimewakuta? Maana wengine ni wasichana wadogo wa shule tayari
wanavitambi wakati mwingine utakuta mama ameongozana na binti yake wote
wanavitambi. Je kuna namana yoyote ya kuwaokoa? Tuwasaidie maana nadhani hali hiyo itakuwa na athari kiafya kwao mbali ya kuharibu maumbile yao(kupoteza shepu)
Siku utasikia Kila Mwanamke hapa mjini anataka
Saturday, 18 January 2014
SIKU HIZI WANAWAKE WANAONGOZA KWA VITAMBI NA MATUMBO MAKUBWA.
12:17
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment