
STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ameamua kumuweka bayana mchumba wake wa sasa
anayejulikana kwa jina la G. Modo baada ya kukaa kimya muda mrefu tangu alipoachana na Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
Akizungumza
na gazeti hili hivi karibuni, Wolper alisema alikuwa kimya kwa muda
mrefu kwa ajili ya kutafakari kwanza maana asingeweza kukurupuka wakati
bado hawajachunguzana tabia vizuri na mpenzi wake huyo.
“Kiukweli
nafurahia sana uhusiano wangu wa sasa na siwezi kusema moja kwa moja
kuwa ndiye mume wangu kwa vile najua kila kitu kinaongozwa na Mungu,
ninachokiomba ni ndoto yangu ikamilike tu kwani nahisi niliyempata ni
sahihi kwangu,” alisema Wolper.
Wolper
aliongeza kuwa kama siku Mungu atajalia kwa mpenzi wake huyu
kitakachofuatia ni kwenda moja kwa moja kwa wazazi wa pande zote mbili
ili kupata baraka na ndiyo kitu ambacho anakiomba kila kukicha.
CREDIT: GPL
Saturday, 18 January 2014
JACKLINE WOLPER AMWANIKA MPENZI WAKE MPYA HADHARANI.
12:28
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment