
ZILE tambo, mbwembwe na majigambo ya Miss Tanzania 2006/07, aliye pia msanii wa filamu Bongo,
Wema
Isaac Sepetu, zimefika mwisho kufuatia kunyang’anywa samani za ofisi
yake ya Endless Fame Film Production na aliyekuwa mpenzi wake, Clement
‘kigogo wa ikulu’ na sasa amebaki mweupe, Amani limepakuliwa ikiwa
imeiva.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo la aibu lilijiri hivi karibuni
kwenye ofisi hiyo ya Wema iliyopo Mwananyamala-Komakoma jijini Dar.
KIGOGO WA IKULU AVAMIA NA MABAUNSA
Habari
za uhakika zinadai kuwa, siku ya tukio, Clement akiwa ameongozana na
watu waliosadikiwa kuwa ni mabaunsa, walivamia ofisi hiyo aliyomfungulia
mlimbwende huyo na kukomba vitu vyote vya thamani alivyomnunulia wakati
wa mapenzi motomoto (hakuna lenye mwanzo lisilo na ncha).
KUMBE ALIKODI CANTER
Kama
njiwa apelekaye ujumbe muhimu wa huba, mtoa taarifa huyo alizidi
kumwaga ‘upupu’ kuwa, siku hiyo Clement mbali na gari lake la kifahari,
pia alitinga akiwa na gari aina ya Canter ambapo bila maswali wala
maelezo achilia mbali ufafanuzi, alikusanya vifaa vyote na kuvirundika
kwenye gari.
IDADI YA VITU VILIVYOBEBWA
Vifaa
hivyo ni tarakishi (computer), kamera ya kurekodi sinema (video
camera), vifaa vya kurekebisha hali ya hewa (air conditioner), vifaa vya
kuhifadhia umeme wa ziada, uninterruptible power supply (ups) pamoja
na vifaa vingine zikiwemo nyaya za umeme na kuiacha ofisi nyeupe kama
uwanja wa mpira.
“Hali
ni mbaya sana, jamaa (Clement) alichukua kila kitu ndani ya ofisi hiyo
kuanzia kompyuta, kamera hata nyaya! Hivi tunavyoongea, ofisi haina kitu
kabisa,” kilisema ‘kikulacho’ hicho.
CHANZO NI DIAMOND
Mpashaji
huyo alizidi kuyapa utulivu masikio ya mwandishi wetu kuwa, chanzo cha
kigogo huyo kufanya ‘umafia’ huo ni kitendo cha Wema kurejesha penzi
lake kwa ‘mtemea maiki’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond
Platnumz’.
Taarifa
hizo zilieleza kuwa, kitendo hicho kilichochea hasira za Clement, hasa
pale Diamond alipohojiwa kuhusu kuingilia penzi hilo na kujibu hamwogopi
mtu, “ndiyo maana Clement akaamua kumwaga ugali baada ya wawili hao
(Wema na Diamond) kumwaga mboga,” kiliongeza chanzo.
HEBU MSIKILIZE WEMA
Ili
kujua yapi ni maziwa na lipi ni tui juu ‘niuz’ hizo, mwandishi wetu
alimtafuta Wema na kukutana naye laivu juzi ambapo alikiri kukumbwa na
zahama hiyo huku akionesha mshangao wa wazi kwa kitendo alichofanyiwa na
‘zilipendwa’ wake huyo
“Ni
kweli kabisa Clement amefanya hivyo, lakini nashangaa na ni mara yangu
ya kwanza kuona wapenzi wakiachana mwanaume anaamua kuchukua vitu vyote
alivyowahi kumnunulia au kumpa.
“Huo ni ushamba na unyanyasaji, akumbuke kwamba alipokuwa na mimi alinitumia pia,” alisema Wema na kuongeza:
“Hata hivyo, namshukuru Mungu, vitu vyote alivyochukuwa Clement, baby (Diamond) kasema ataninunulia, wiki mbili hazitapita.”
Wema
alikwenda mblele zaidi kwa kuonesha machungu yake kwa kigogo huyo pale
aliposema: “Kwanza nasikia vitu vyenyewe alipofika nyumbani kavimwaga
nje maana ndani hakuna nafasi.”
KAANZA MWAKA VIBAYA
Mwanzoni
mwa mwaka huu, Wema alikumbwa na mkasa wa kunyang’anywa lile gari la
kifahari alilodai ni lake, Audi Q7 baada ya kusemekana kuwa halikuwa
lake.
Kumbe
gari hilo alipewa na Clement ambaye naye alilikopa kwa thamani ya
shilingi milioni 90 kutoka kwa mtu aliyejulikana kwa jina la Shadrack
Tweve.
Tweve,
baada ya kuzungushwa sana kulipwa fedha hizo, alikimbilia Mahakama ya
Wilaya ya Ilala ambapo hakimu aliamuru gari hilo likamatwe na
kurejeshewa mlalalamikaji huyo.
PENZI LA WEMA, KIGOGO WA IKULU
Uhakika
ni kwamba, penzi kati ya Wema na kigogo huyo halipo tena na kwa sasa
jamaa ana demu mwingine (jina tunalo) ambapo mapaparazi wetu wanaendelea
kufuatilia kwa karibu ili kuwanasa katika mazingira yoyote yale.
Saturday, 18 January 2014
WEMA ANYANG'ANYWA KILA KITU, KISA KURUDIANA NA DIAMOND.
12:28
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment